HRW yasema mauaji ya kutisha yanatokea Darfur
11 Julai 2023Shirika jingine la DBA linalofuatilia mzozo wa Sudan limeeleza katika taarifa yao kuwa katika mji mkuu wa jimbo la Magharibi la Darfur, El Geneina, watu kadhaa wameuawawa katika siku za hivi karibuni huku maiti zikitapakaa barabarani.
Mashahidi wameripoti mashambulizi yanayofanywa na wanamgambo wa Kiarabu na Kikosi cha Msaada wa Dharura (RSF) dhidi ya watu wasiokuwa Waarabu kutoka jamii ya Masalit, ambayo ndio jamii kubwa katika mji huo.
Soma zaidi: Guterres alaani shambulio la anga lililowaua watu 22 Sudan
Wahariri wa Ujerumani wazungumzia mzozo wa Darfur
Hali hiyo imeongeza wasiwasi na kusababisha maelfu ya watu kukimbilia karibu na mpaka wa Chad.
Katika ripoti yao mpya, Human Rights Watch imeorodesha mauaji ya watu wasioupungua 40, ikiwa ni pamoja na mauaji ya jumla ya wanaume 28 wa makabila yasiyokuwa ya Kiarabu katika mji wa Misteri ulioko kilomita 28 kutoka El Geneina.
Shirika la Human Rights Watch limeitaka Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) kuchunguza mauaji hayo.