Baada ya Shirika la kimataifa la kutetea haki za binaadamu la Human Rights Watch kusema kuwa serikali ya Tanzania inapaswa kuchukua hatua madhubuti ili kuondoa hali ya kuzorota kwa hali ya haki za binaadamu kabla ya uchaguzi . DW imezungumza na Profesa Palamagamba Kabudi, huyu ni waziri wa sheria na katiba wa Tanzania msikilize akielezea kuhusu ripoti hiyo.