HRW: RSF wanaweza wakawa wamefanya mauaji ya halaiki Sudan
9 Mei 2024Vikosi vya wanamgambo vya (RSF), pamoja na washirika wao, kwa sehemu kubwa wanashutumiwa kwa mauaji ya kikabila, uhalifu dhidi ya ubinadamu na uhalifu wa kivita katika vita vyao na jeshi la Sudan, vilivyoanza Aprili 2023.
Wanasheria wa haki za binadamu katika maeneo hayo wameelezea kufuatilia namna ambapo wapiganaji walilenga "wanachama mashuhuri wa jumuiya ya Massalit", wakiwemo madaktari, watetezi wa haki za binadamu, viongozi wa eneo hilo na maafisa wa serikali.
Soma pia:RSF: Serikali hazifanyi jitihada za kutosha kuunga mkono uhuru wa habari
Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa vita hivyo vimesababisha vifo vya maelfu, wakiwemo hadi watu 15,000 katika mji wa El-Geneina wa Darfur Magharibi.
Eneo hilo ndilo lengo la ripoti ya Human Rights Watch yenye kurasa 186 iliyojikita katika Mauwaji ya Kikabila na Uhalifu Dhidi ya Ubinadamu huko Darfur Magharibi.