1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

HRW: Jeshi la Chad lilihusika na vifo vya waandamanaji

8 Agosti 2024

Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch limesema kuwa jeshi la Chad lilihusika na vifo vya watu waliokamatwa baada ya maandamano ya Oktoba 2022.

https://p.dw.com/p/4j9dO
Wanajeshi wa Chad wakiwa na wenzao wa Ufaransa
Wanajeshi wa Chad wakiwa na wenzao wa UfaransaPicha: Sebastien Rieussec/Hans Lucas/IMAGO

 Takriban watu wanne walifariki dunia walipokuwa wakipelekwa katika gereza la Koro Toro na wengine sita walikufa ndani ya gereza.

Ripoti ya Human Rights Watch imeeleza kuwa haifahamiki ni wapi alipofia mtu mwingine aliyekuwa akishikiliwa pia.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa huenda idadi ya waliokufa ni kubwa zaidi katika maandamano hayo yaliyofanyika kupinga kurefushwa kwa utawala wa kiongozi wa mpito wa Mahamat Deby Itno. 

Soma pia:Chad yatangaza serikali mpya baada ya utawala wa kijeshi

Mamia ya watu walikamatwa na kupelekwa kwenye gereza la Koro Toro lililo umbali wa kilomita 600 kutoka mji mkuu wa Chad, N'djamena.

Shirika la Human Rights Watchlilizitaka mamlaka za Chad, Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa kuchungunza kilie lilichokiita kuwakamata watu hao kinyume cha sheria, na vifo vya waandamanaji mikononi mwa polisi.