1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

HRW: 2023 ulikuwa mwaka wa ukandamizaji mkubwa wa haki

Sylvia Mwehozi
12 Januari 2024

Ripoti mpya iliyotolewa na Shirika la kimataifa la haki za binadamu la Human Rights Watch, inasema mwaka 2023 kulishuhudiwa ukandamizaji mkubwa wa haki za binadamu.

https://p.dw.com/p/4b9OW
Human Rights Watch
Nembo ya shirika la Human Rights Watch Picha: John MacDougall/AFP/Getty Images

Ripoti mpya iliyotolewa na Shirika la kimataifa la haki za binadamu la Human Rights Watch, inasema mwaka 2023 kulishuhudiwa ukandamizaji mkubwa wa haki za binadamu, huku viongozi wa ulimwengu wakipuuza ukiukwaji huo nchini Sudan na Gaza na dhidi ya jamii ndogo ya Uyghurs.

Soma: Umoja wa Mataifa wabaini dalili za uhalifu wa kivita katika vita vya Gaza

Katika ripoti yake ya dunia ya mwaka 2024, Human Rights Watch imetaja mateso makubwa yaliyosababishwa na vita vya Israel dhidi ya Hamas, migogoro ya Ukraine, Myanmar, Ethiopia na eneo la Sahel barani Afrika.

Mkurugenzi wa shirika hilo kanda ya Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini Lama Fakih, amesema endapo mienendo ya kutisha ya ukiukwaji wa haki za binadamu haitadhibitiwa, itaitumbukiza eneo hilo katika machafuko zaidi na athari za kimataifa.

Ripoti hiyo pia imegusia uharibifu uliochangiwa na mabadiliko ya Tabia Nchi na ukosefu wa usawa wa kiuchumi.