Hosni Mubarak ashinikizwa ajiuzulu
26 Januari 2011Matangazo
Kwa mujibu wa afisa mmoja wa usalama aliyeko kwenye mji wa bandari wa Suez,waandamanaji hao waliuawa pale ghasia zilipozozuka katika yao na maafisa wa polisi.Afisa huyo mmoja wa polisi aliuawa baada ya kujeruhiwa katikati ya mji mkuu wa Misri wa Cairo,kulikofanyika maandamano ya kumtaka Rais Hosni Mubarak ajiuzulu.Kulingana na kiongozi wa kundi la Muslim Brotherhood lililopigwa marufuku,Gamal Heshmat,raia hawana imani na uongozi uliopo.
Mwanasiasa huyo wa upinzani alisisitiza kuwa ijapokuwa serikali imeahidi itafanya mageuzi,hatua bora ni kujizulu.
Polisi wa kupambana na ghasia walilazimika kuwafyatulia mabomu ya gesi ya machozi maelfu ya waandamanaji ambao wengi wao ni vijana waliorusha mawe na kupiga mayowe.