1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hezbollah yashambulia maeneo ya Israel

4 Julai 2024

Kundi la Hezbollah nchini Lebanon linaloiunga mkono Iran, limesema limerusha makombora 200 na droni katika maeneo ya kaskazini mwa Israel hii leo, kulipiza kisasi mauaji ya kamanda wao mmoja Jumatano.

https://p.dw.com/p/4hsQh
Mashambulizi ya Israel na Hezbollah
Israel limesema makombora 200 yaligunduliwa kuvuka kutoka Lebanon kuelekea upande wa IsraelPicha: Ayal Margolin/REUTERS

Kulingana na vyanzo vya usalama vya Lebanon, shambulio hilo la Hezbollah lilikuwa moja kati ya mashambulizi makali zaidi tangu mapigano yalipoanza katika mpaka kati ya Lebanon na Israel mnamo Oktoba 8.

Soma pia: Israel yasema wanajeshi wake 18 wamejeruhiwa katika shambulio la Hezbollah

Katika taarifa, kundi hilo limesema kuwa kama sehemu ya jibu la shambulizi na mauaji yaliofanywa na adui wake katika eneo la Al-Housh mjini Tyre, lilifanya mashambulizi hayo huku likiongeza kuwa makombora yake yalilenga kambi kadhaa za jeshi la Israel.

Jeshi la Israel limesema takriban makombora 200 yaligunduliwa kuvuka kutoka Lebanon kuelekea eneo la Israeli, baadhi yakatunguliwa na mfumo wa ulinzi wa anga pamoja na ndege za kivita.