1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroLebanon

Hezbollah yafyetua makombora kuelekea Israel

6 Januari 2024

Kundi la wanamgambo wa Hezbollah la nchini Lebanon limefyetua makombora kadhaa kuelekea kaskazini mwa Israel Jumamosi na kusema hiyo ni awamu ya kwanza ya kulipa kisasi.

https://p.dw.com/p/4avKY
Lebanon imewasilisha malalamiko kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kufuatia mauaji yaliyolengwa na Israel
Lebanon imewasilisha malalamiko kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kufuatia mauaji yaliyolengwa na Israel Picha: AFP

Mashambulizi hayo yamefanywa siku moja baada ya kiongozi wa Hezbollah, Sayyed Hassan Nasrallah kusema kundi hilo litajibu mauaji ya naibu kiongozi wa kundi la Hamas Saleh Arouri yaliyofanywa kwa shambulizi la droni linaloshukiwa kupangwa na Israel.

Kundi hilo limearifu kwamba makombora 62 yamefyetuliwa kuilenga kambi ya jeshi la anga ya Israel ya Mount Meron na kwamba limefanikiwa kuyapiga maeneo yaliyokusudiwa.

Kwa upande wake Jeshi la Israel limesema limerikodi makombora 40 yaliyolilenga eneo la Meron lakini halikusema chochote kuhusu mashambulizi dhidi ya kambi ya jeshi.

Makabiliano hayo ya mpakani yanayochochewa na kampeni ya kijeshi ya Israel huko Gaza na dhidi ya kundi la Hamas yanazidisha wasiwasi wa kusambaa kwa mzozo kwenye kanda nzima ya Mashariki ya Kati.