1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

HELSINKI: Ujenzi wa makazi ya Wayahudi usitishwe

7 Septemba 2006
https://p.dw.com/p/CDEj

Umoja wa Ulaya umetoa mwito kwa Israel isitishe mpango wake wa kutaka kuongeza nyumba za walowezi wa Kiyahudi kwenye Ukingo wa Magharibi.Rais wa Halmashauri ya Umoja wa Ulaya ambayo hivi sasa inaongozwa na Finnland,amesema mpango huo unakiuka sheria ya kimataifa.Israel imetangaza kuwa inataka kujenga kama nyumba 700 zingine katika makazi ya Wayahudi,sehemu za mashariki na kusini ya Jerusalem.Mradi huo unahusika na ujenzi mkubwa kabisa wa makazi ya Wayahudi,tangu waziri mkuu Ehud Olmert kushika madaraka mwanzoni mwa mwezi Mei.