1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Helikopta mbili zagongana Libya Mashariki

20 Septemba 2021

Vikosi tiifu kwa kamanda wa Libya vimesema ndege mbili za kijeshi zimegongana katika eneo la Mashariki katika kijiji cha Msus na kuwaua maafisa wawili.

https://p.dw.com/p/40YPp
Libyen Konflikt l dem libyschen General Khalifa Haftar treue Kämpfer
Picha: Getty Images/AFP/A. Doma

Vikosi vya Majeshi ya Kiarabu vya Libya, vinavyoongozwa na Jenerali Khalifa Haftar vimesema helikopta mbili ziligogangana Jumapili kwenye kijiji hicho kilichoko kusini mashariki mwa mji wa Benghazi.

Taarifa fupi ya vikosi hivyo imeeleza kuwa maafisa wawili ambao ni wafanyakazi kwenye helikopta moja, akiwemo Brigedia Jenerali Bouzied al-Barrasi wamekufa katika ajali hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, wafanyakazi katika helikopta ya pili wamesalimika. Taarifa hiyo haijaelezea chanzo cha ajali hiyo, ingawa imesema kuwa helikopta hizo zilikuwa kwenye operesheni ya kijeshi.

Mohammad Younes Menfi, mkuu wa Baraza la Urais la Libya, ameomboleza vifo vya maafisa hao wawili. Vikosi vya Haftar vinadhibidi eneo la mashariki na sehemu kubwa ya kusini mwa Libya.

Ajali hiyo imetokea wakati vikosi hivyo vikipambana na wapiganaji wa Chad kwenye maeneo ya kusini mwa Libya yanayopakana na Chad.