1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAfrika Kusini

Hatima ya kisiasa wa rais Ramaphosa iko matatani

2 Desemba 2022

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amekuwa akikabiliwa leo na wito wa kujiuzulu baada uchunguzi wa bunge kubaini kuwa huenda alikiuka sheria za nchi.

https://p.dw.com/p/4KP2y
UK, London | Cyril Ramaphosa, Präsident von Südafrika
Picha: Justin Tallis/AFP/Getty Images

Hatima ya kisiasa wa Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa iko gizani huku raia wa nchi hiyo wakijiuliza iwapo atang'ang'ania madarakani au kujiuzulu kwa tuhuma zinazomkabili.

Kufuatia shinikizo linalomtaka rais huyo ajiuzulu kuendelea kuzua mjadala mkubwa nchini humo, ripoti kutoka ikulu ya Afrika Kusini zinasema, Rais Ramaphosa yuko kwenye mashauriano na watu wake wa karibu, juu ya uamuzi wa kujiuzulu kutokana na ripoti ya uchunguzi kuonesha alivunja katiba ya nchi.

Taarifa za rais huyo za kufanya mashauriano na watu wake wa karibu, zilianza kuzagaa jana Alhamis baada ya ripoti kutoka kwa jopo la wataalamu wa sheria kudai kwamba rais huyo alificha dola milioni nne pesa taslimu katika shamba lake mwaka 2020.

Alipoulizwa nini hatma ya Rais Ramaphosa, msemaji wa Ikulu Vincent Magwenya alisema mashaurino hayo hayahusiani na chaguo gani linafaa zaidi kwa Rais, bali kinachojadiliwa ni hatua gani ya kuchukua itakayokuwa na manufaa kwa nchi.