1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hasira zatawala Tunisia baada ya kifo cha mtu mmoja

5 Julai 2023

Vijana nchini Tunisia wametoa miito ya kulipa kisasi kufuatia kifo cha mwanaume mmoja raia wa nchi hiyo aliyeshambuliwa kwa kisu wakati wa vurumai iliyozuka kati ya wenyeji wa mji wa mwambao wa Sfax.

https://p.dw.com/p/4TRYA
Wahamiaji Tunisia
Wahamiaji wa Tunisia wakijaribu kuvuka bahari kuingia UlayaPicha: Hasan Mirad/Zumapress/picture alliance

Vijana nchini Tunisia wametoa miito ya kulipa kisasi kufuatia kifo cha mwanaume mmoja raia wa nchi hiyo aliyeshambuliwa kwa kisu wakati wa vurumai iliyozuka kati ya wenyeji wa mji wa mwambao wa Sfax na wahamiaji kutoka mataifa ya kusini mwa jangwa la Sahara.

Miito hiyo iliyoambatana na kauli za kibaguzi imesikika wakati wa mazishi ya mwanaume huyo yaliyofanyika jana baada ya kifo chake kutokea kwenye mapambano kati ya mwenyeji na wageni Jumapili iliyopita.

Polisi ya Tunisia imesema washukiwa watatu wote wakiwa na asili ya Cameroon wamekamatwa kuhusiana na kisa hicho. Mji wa Sfax ambao ndiyo wa pili kwa ukubwa nchini Tunisia umekuwa lango la wahamiaji wa nchi za kiafrika wanaojaribu kuingia Ulaya.

Wenyeji wa mji huo wamekuwa wakipinga uwepo wa wahamiaji na mara kadhaa wametumbukia kwenye uhasama na mapambano yanayosababisha hasara na kujeruhiwa kwa watu.