1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Harris, Trump kufanya kampeni zao huko mjini Milwaukee

1 Novemba 2024

Donald Trump na Kamala Harris wanafanya leo mikutano ya kampeni katika mji mkubwa kabisa wa jimbo la Wisconsin nchini Marekani, Milwaukee.

https://p.dw.com/p/4mTqA
 Kamala Harris na Donald Trump
Kamala Harris na Donald Trump Picha: David Swanson/Mike Blake/REUTERS

Donald Trump na Kamala Harris wanafanya leo mikutano ya kampeni katika mji mkubwa kabisa wa jimbo la Wisconsin nchini Marekani, Milwaukee. Wagombea wote wawili wanafanya kampeni za dakika za mwisho kuwavutia wapiga kura zikiwa zimesalia siku nne kabla Uchaguzi wa Rais.

Mrepublican anarejea kwenye ukumbi ambao alipewa tiketi ya chama chake kugombea urais. Kinyang'anyiro cha kutafuta kura katika majimbo hayo yanayoegemea zaidi chama cha Democratic kimejiri baada ya wagombea hao kufanya kampeni hapo jana katika majimbo ya Magharibi mwa Marekani.

Soma: Kamala Harris amshambulia Trump katika mkutano wake wa kwanza wa hadhara

Harris alikuwa na mkutano mkubwa jimboni Las Vegas wakati Trump akiwa jimboni Arizona. Kiasi ya watu milioni 63.5 wamepiga kura mapema, ikiwa ni zaidi ya asilimia 40 ya jumla ya kura zilizopigwa mwaka wa 2020. Uchaguzi wa Marekani utafanyika Jumanne ijayo Novemba 5.