HARARE: Polisi wazuia pesa na mali za magendo
24 Mei 2005Matangazo
Polisi nchini Zimbabwe wamewakamata kama watu 10,000 katika mji mkuu Harare katika opresheni ya kuwaondosha wahalifu.Kwa mujibu wa msemaji wa polisi,pesa na bidhaa zenye thamani ya zaidi ya Euro 100,000 zimezuiliwa.Biashara ya magendo imestawi nchini Zimbabwe wakati asili mia 80 ya watu wasio na ajira wakihangáika kuendesha maisha yao.Zimbabwe inakabiliwa na upungufu mkubwa wa vitu vya kawaida kama chakula na mafuta ya petroli.