Harakati za uasi Jamhuri ya Afrika ya Kati zaongezeka
18 Juni 2024Wataalamu hao wa Umoja wa Mataifawameweka wazi ripoti zilizothibitishwa za uvamizi wa anga uliofanyika na jeshi la Sudan karibu na maeneo ya mipakani na wanamgambo wa kundi la RSF kuvuka na kuingia nchini humo ili kusajili wapiganaji zaidi kutoka Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Umoja wa Mataifa umeorodesha karibu wakimbizi 10,7000 wa Sudan ambao wamekimbia makwao mwishoni mwa mwezi Machi.
Soma pia: Ufaransa yapeleka wanajeshi zaidi Mali
Imeongeza kuwa, wakimbizi wapya 565, wengi wao wakiwa wanawake na watoto, wanawasili katika kambi ya wakimbizi ya Korsi iliyoko katika mji wa kaskazini wa Birao kila wiki.
Sudan ilitumbukia kwenye mzozo katikati ya mwezi Aprili mwaka jana kufutia msuguano kati ya kiongozi wa jeshi Jenerali Abdel Fattah al-Burhan na wanamgambo wa RSF chini ya Jenerali Mohamed Hamdan Dagalo.