1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Haniyeh wa Hamas kuzikwa leo Qatar

Angela Mdungu
2 Agosti 2024

Qatar leo inatarajiwa kufanya mazishi ya kiongozi wa Hamas, Ismail Haniyeh, baada ya mauaji yake huko Tehran, katika shambulizi linalodaiwa kufanywa na Israel, jambo lililosababisha hatari ya kuenea kwa machafuko.

https://p.dw.com/p/4j2AM
Iran I Mazishi ya kiongozi wa kisiasa wa Hamas Ismail Haniyeh huko Tehran
Watu wakihudhuria hafla ya mazishi ya aliyekuwa kiongozi wa Hamas Ismail Haniyeh, ambaye aliuawa Tehran, Iran Agosti 1, 2024.Picha: Iranian Leader Press OfficeAnadolu/picture alliance

Haniyeh atazikwa katika maziara ya Lusail, kaskazini mwa Doha baada ya sala itakayofanywa katika msikiti mkubwa nchini Qatar wa Imam Muhammad bin Abdul Wahhab. Hamas imesema kwamba viongozi wa Kiarabu na Kiislamu, pamoja na wawakilishi wa makundi mengine ya Palestina na raia, watahudhuria mazishi hayo. Kuuwawa kwa Haniyeh kulifanyika masaa machache tu baada ya Israel kufanya shambulizi kusini mwa Beirut na kumuua Fuad Shukr, kamanda wa kijeshi wa kundi la Hezbollah lililo na mafungamano na Hamas.