1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hamna usalama timamu katika usafiri wa anga

Miraji Othman28 Desemba 2009

Ugaidi unapenya katika vizuizi vya misafara ya ndege

https://p.dw.com/p/LFXh
Hospitali katika Ann Arbor huko Michigan, Marekani, ambako Farouk Abdulmuttalib anatibiwa kutokana na mrpuko alioupata kutokana na chombo aliochovaa mwilini.Picha: AP

Huko Marekani, ndege iliojaa abiria, chupu chupu ilinusurika kuripuliwa. Kijana wa Ki-Nigeria, mwenye umri wa miaka 23, alitaka kuiripuwa hewani ndege hiyo iliokuwa ikitokea Amsterdam kwendea Detroit, Marekani. Licha ya usimamizi, uchunguzi na ukaguzi wote mkali wa usalama, kijana huyo alifaulu kuingia ndani ya ndege hiyo na baruti. Vipi imewezekana, anauliza Ralph Sina wa kutoka hapa Deutsche Welle. Uhariri wake unasomwa studioni na Othman Miraji...

Usalama ni suala la kimwazo, ambalo sisi wanadamu tunapenda kuliamini, lakini katu haliwezi kuweko. Hakuna ulinzi ulio kamili dhidi ya magaidi na wale wanaojiita wanachama wa mtandao wa al-Qaida. Na jambo hilo limedhihirika upya katika mkasa wa ndege ya shirika la Delta Nambari 253 iliokuwa ikisafiri kutokea Amsterdam kuendea Detroit, Marekani. Mwanafunzi wa taaluma ya ujenzi wa mashine, aliye na umri wa miaka 23, bila ya shida, aliweza, tena bila ya kubughudhiwa, kuingia ndani ya ndege hiyo pamoja na huenda na baruti za miripuko, au kwa vyovyote na mchanganyiko wa vitu vya hatari vyenye kuripuka na kusababisaha moto. Aliweza kuingia na vitu hivyo bila ya wasiwasi ndani ya ndege ya shirika la Kiholanzi la KLM huko Lagos, Nigeria. Hilo sio jambo la kushangaza sana, kwani yeyote anayevijuwa viwanja vya ndege vya kimataifa katika Afrika, basi anatambuwa kwamba viwanja hivyo sivyo ambavyo vina ulinzi ulio bora kabisa duniani. Na hapo mtu anajiuzuwia kusema zaidi.

Mashirika ya ndege ya Ulaya na ya Kimarekani yanatambua kasoro hiyo na mara nyingi huweka wafanya kazi wao wenyewe wa usalama katika viwanja vya ndege kutokea Afrika. Ni sawa kama ni huko Kenya, ambako mwaka 1998 mtandao wa al-Qaida uliuripuwa ubalozi wa Marekani mjini Nairobi, au huko Nigeria, ambako mtandano wa al-Qaida mara nyingi unapata wafuasi zaidi miongoni mwa Waislamu wa nchi hiyo. Lakini mkasa wa juzi wa huyu kijana wa Ki-Nigeria, Farouk Abdul Muttalib, umerdhihirisha kwamba hatua zote hizi za ziyada za ulinzi hazijaweza kufanya kazi.

Na hiyo sio tu katika Afrika, lakini pia huko Marekani na hapa Ulaya. Farouk Abdul Muttalib aliweza bila ya shida kubadilisha ndege mjini Amsterdam, kutoka ndege ya shirika la KLM na kuingia katika ile ya shirika la Kimarekani la Delta kuelekea Detroit. Hamna mtu aliyemzuwia, hamna mtu aliyemchunguza vilivyo.

Yaonesha makampyuta na idara za upelelezi, licha ya janga lililotokea Septemba 11 huko Marekani, bado hayajafungamana vizuri katika mtandao, ama sivyo basi maafisa wa forodha wa Uholanzi wangebidi wachunguze katika kompyuta zao. Kwani maelezo juu ya mwanafunzi huyo wa uhandizi wa Ki-Nigeria inasemakana yalikuwemo katika kompyuta za idara za upelelezi za Marekani kama mtu ambaye anaweza kuwa gaidi wa hatari, japokuwa jina lake halikuwemo katika ile orodha ya watu wanaosakwa sana na viwanja vya ndege vya Kimarekani na mashirika ya ndege kuwa ni mshukiwa wa ugaidi.

Mkasa wa Farouk Abdul Muttalkib unaonesha vipi wakala mbali mbali za upelelezi duniani zinafanya kazi bila ya wakala mmoja kujuwa mwengine unafanya nini. Ndio maana M-Nigeria huyo aliweza kujifunga na baruti hiyo ya unga ndani ya mwili wake pamoja na maji ya kuripuwa baruti hiyo, tena ndani ya ndege ya chapa ya Aibus iliosheheni karibu abiria 300. Mkasa wake unadhihirisha kwamba uchunguzi wote wa kina wa viatu, mifuko na kompyuta za Laptop za abiria, uchunguzi wote wa usalama wa kugundua vyuma na unga wa miripuko katika mizigo ya abiri kwenye viwanja vya ndege hausaidii sana, pindi vifaa hivyo vya magaidi vitavaliwa mwilini na kuwa karibu sana na ngozi ya abiria. Hakuna chombo cha kugundua chuma kinaweza kufanya kazi, kwa vile hapo hakuna chuma.

Lakini kukiweko uchunguzi wa kwenda mbali zaidi ya hapo, basi usafiri wa ndege wa kimataifa utazorota; hiyo itamaanisha idara za upelelezi katika viwanja vya ndege zitafanya kama vile nyingi zinavopenda kufanya. Badala ya kila abiria kuchunguzwa kidogo, yawezekana abiria fulani wa ndege wakachunguzwa zaidi kutokana na nchi wanazotokea na kutokana na maelezo yao ya kibinafsi. Lakini jambo hilo litahitaji ujasiri wa kisiasa ambao hauko sio Marekani wala hapa Ulaya. Na ndio maana ule usalama unaowezekana kuwekwa na mwanadamu dhidi ya shambulio la kigaidi hewani na ardhini utabakia tu kuwa ni jambo la kuwaza.

Mwandishi:Othman Miraji-ZPR-Ralph Sina

Mhariri:Mwadzaya thelma