MigogoroMashariki ya Kati
Hamas yakanusha kujiondoa kwenye mchakato wa mazungumzo
14 Julai 2024Matangazo
Kundi hilo limesema mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja bado yanaendelea licha ya mamlaka ya afya inayodhibitiwa na kundi hilo kusema kuwa mashambulizi ya anga ya Israel yaliwauwa watu 90 jana Jumamosi.
Awali, Israel ilisema kuwa mashambulizi hayo yalimlenga kiongozi wa tawi la kijeshi wa Hamas, Mohammed Deif. Hata hivyo muwakilishi wa kundi hilo katika mji Mkuu wa Lebanon, Beirut amesema leo kuwa, Deif hakuuwawa katika tukio hilo.
Hayo yakijiri, Jeshi la Israel limesema kuwa limemuuwa kamanda wa kikosi cha kijeshi cha Hamas katika mji wa Khan Younis Rafa Salama, katika shambulio la anga la Jumamosi. Shambulio hilo ndilo lililotajwa kumlenga kiongozi wa tawi la kijeshi wa Hamas, Mohammed Deif.