1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hali ya mambo yazidi kuwa tete nchini Madagascar

17 Machi 2009

Umoja wa Ulaya waonya kuutenga utawala utakaoingia madarakani kimabavu

https://p.dw.com/p/HDqI
Kiongozi wa upinzani Andry Rajoelina aungwa mkono na jeshiPicha: picture-alliance/ dpa

Wanajeshi nchini Madagascar wameyateka makaazi ya rais pamoja na benki kuu ya taifa.Hatua hiyo inatajwa kama ni mpango wa kumhujumu rais Ravalomanana katika mvutano wa kuwania madaraka kati yake na kiongozi wa upinazani Andry Rajoelina.

Maafisa wa kijeshi wamewaambia waandishi wa habari kwamba idadi kubwa ya wanajeshi sasa wanamuunga mkono Rajaelina.

Umoja wa Ulaya ukizungumzia juu ya mzozo huo wa kisiasa umeonya dhidi ya matumizi ya nguvu kuipindua serikali iliyoko madarakani.

Waziri wa mambo ya nje wa jamhuri ya Czech inayoshikilia wadhifa wa kupokezana wa Mwenyekiti wa Umoja wa Ulaya Karel Schwarzenberg amesema Umoja wa ulaya unapinga matumizi ya nguvu na ikiwa jeshi litakiuka katiba Umoja huo utachukua hatua kama iliyochukuliwa dhidi ya Mauritania.

Kiongozi wa upinzani nchini Madagascar Andry Rajoelina ametoa mwito kwa jeshi kumkamata rais lakini rais Ravalomanana alikuwa yuko katika makaazi yake mengine nje ya mji mkuu Antananarivo.

Rais huyo wa Madagascar amependekeza kufanyike kura ya maoni ili kutoa nafasi wananchi kuamua nani aiongoze nchi hiyo.Rajoelina amekataa pendekezo hilo.

Mwandishi:Saumu Mwasimba/ZR