Hali ya maambukizi imekuwa mbaya nchini India
27 Aprili 2021Kansela Angela Merkel na mawaziri wakuu wa majimbo 16 ya Ujerumani wamekubaliana kukamilisha zoezi la utoaji chanjo ya kitaifa kwa makundi maalumu yaliopewa kipaumbe kwa zingatio la umri ifakapo Juni.
Akizungumza na waandishi wa habari katika kile kilichoitwa mkutano wa kilele wa chanjo, Merkel alisema hatua hiyo haimaanishi kwamba kila mtu atakuwa amechanjwa, lakini kila mtu anaweza kuomba fursa ya kuchanjwa. Na wataweza kuipata kwa zingatio la usambazaji wake.
Hatua hiyo imetokana na jitihada ya usambazaji bora wa chanjo kwa makundi hayo, na kwamba Merkel na mawaziri wakuu wa majimbo wana matumaini zoezi la utoaji chanjo kwa upande huo linaweza kuhitimishwa Mei.
Tangu kuzuka kwa janga la virusi vya coronazaidi ya mwaka mmoja uliopita Ujerumani, imerekodi visa milioni 3.3 na kwamba asilimia 23 ya Wajerumani wamechanjo japo dozi moja na nyingine 7.2 wamekamilisha dozi kamili.
Msaada wa haraka unahitajika katika kuwanusuru raia wa India
Katika hatua nyingine Marekani na Uingereza zimechukua juhudi za haraka za kuisaidia India mashine za kupumulia na vifaa vya chanjo, baada ya hali ya taifa hilo kuelezwa na Shirika la Afya Duniani kuwa mbaya zaidi, huku Italia ikianza kuondosha vizuizi vya kukabiliana na janga la Covid-19.
India yenye idadi ya watu bilioni 1.3, inapambana na ongezeko kubwa la maambukizi, na hospitali zimezidiwa ambapo pia vituo vya kuchoma maiti kama utaratibu wa mazishi ya Kiindi, vinafanya kazi hiyo kwa wakati wote. Kwa rekodi za jana Jumatatu kwa mfano, kumekuwa na maambukizi mapya 352,991 na vifo 2,812. Kiwango hicho kikitajwa cha juu zaidi kuwahi kutokea tangu kuzuka kwa janga la virusi vya coroa.
Watalii wa Marekani hivi karibuni watapata ruhusa ya kuingia Ulaya
Watalii kutoka Marekani hivi punde watapata fursa ya kuitembelea Ulaya kwa mara nyingine,ikiwa ni zaidi ya mwaka mmoja baada ya Umoja wa Ulaya kuweka vizuizi kwa mataifa yake 27 ya kanda hiyo, kwa lengo la kudhibiti viruvi vya corona.
Kamisheni ya Umoja wa UIaya, itatoa pendekezo hivi karibuni kwa matiafa wanachama, ingawa taarifa husika haijasema lini safari hizo zinaridhiwa au kwa taratibu zipi. Lakini Jumapili gazeti la New York Time lilimnukuu Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya, Ursula von der Leyen akisema watalii wa Marekani ambao watakuwa wamechanjwa dhidi ya gonjwa la Covid-19 wataruhusiwa kuingia katika mataifa ya Ulaya katika miezi ijayo.
Brazil imekuwa tafa lingine linalilozua kuingizwa kwa chanjo ya Urusi, Sputnik V kwa kutoa sababu ya kuhitaji muda wa kujiridhisha kutokana na hofu ya usalama wake. Huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kumelazimika kusambaza chanjo yake ya AstraZeneca kwa mataifa mengine ya Afrika ili isiharibike kutokana na kucheleweshwa kwa zoezi la usambazaji. Kuchelewa huko pia kunatokana na wasiwasi wa usalama wa chanjo husika.
Chanzo DPA/FP/AP/RTR