Hakuna tuzo za Ballon d'Or mwaka huu kutokana na COVID-19
20 Julai 2020Watayarishaji 'Jarida la michezo la Ufaransa', wamesema leo Jumatatu (20.07.2020) kuwa kutomalizika kwa baadhi ya ligi pamoja na kuahirishwa kwa michuano ya Euro 2020 pamoja na Copa America hakukuweza kuruhusu upigaji kura wa haki.
"Matukio ambayo ni ya kipekee, maamuzi ya kipekee," taarifa ya France Football imesema. "Mwaka kama huu wa aina yake hauwezi , na haupaswi , kuwa kama mwaka wa kawaida."
Ballon d'Or hutolewa katika kura inayopigwa miongoni mwa waandishi wa habari za michezo. Kati ya mwaka 2010 na 2015 France Football iliunganisha nguvu zake na shirikisho linaloangalia mchezo wa kandanda FIFA pamoja na tuzo hiyo lakini makundi hayo mawili yalijitenga kutoa zawadi zao tena mwaka 2016.
Lionel Messi wa Barcelona ni mshindi mara nyingi zaidi akiwa na tuzo sita.
France Football imesema kuwa Ballon d'Or itarejea tena mwaka 2021.