1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mazungumzo ya Syria yaahirishwa mjini Geneva

Mjahida 25 Machi 2016

Wakati mazungumzo ya amani ya Syria yakiakhirishwa baada ya kufanyika kwa siku 10, bado hakuna dalili yoyote ya kupatikana suluhu ya kudumu katika mzozo huo.

https://p.dw.com/p/1IJoD
Genf Friedensverhandlungen zu Krieg in Syrien - Staffan de Mistura mit Bashar al Jaafari
Mjumbe wa serikali katika mazungumzo ya Syria Bashar al Jafari na mjumbe wa UN Staffan de MisturaPicha: Reuters/J. M. Ferre

Mpango wa mjumbe wa Umoja wa Mataifa kwaajili ya Syria Staffan de Mistura ni kuwepo kipindi cha mpito wa kisiasa nchini Syria.

Licha ya kwamba de Mistura alifanikiwa kudhibiti mazungumzo hayo kati ya wajumbe wa serikali na wale wa upinzani, hakuweza kufanikiwa zaidi kuziweka pande hizo zinazohasimiana katika meza moja ya mazungumzo au kujadili ajenda ya baraza la usalama la umoja wa mataifa la kutaka uwepo wa kipindi cha mpito wa kisiasa.

Aidha de Mistura amesema kufuatia mashambulio ya kigaidi yaliyotekelezwa na wanamgambo wa dola la kiislamu nchini ubelgiji na kusababisha mauaji ya zaidi ya watu 30, inaonesha kuwa njia moja ya kuushinda ugaidi ni kuutafutia ufumbuzi mgogoro wa Syria.

Baada ya mapigano nchini humo kuingia mwaka wake wa tano na kila upande katika mzozo huo ukishindwa kuwadhibiti wenzao kijeshi, pande hizo zinazohasimiana zimeamua kuwa hakuna njia nyengine ya kusuluhisha mgogoro isipokuwa mazungumzo.

Schweiz Syrien-Friedensgespräche in Genf
Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kwaajili ya Syria Staffan de MisturaPicha: Reuters/R. Sprich

Hata hivyo Urusi na Marekani wanaounga mkono mazungmzo hayo wanashirikiana pamoja kutafuta suluhu ya kisiasa katika vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyosababisha zaidi ya watu 250,000 kuuwawa huku wengine wengi wakiachwa bila makaazi.

Wanamgambo wa IS washambuliwa katika mji wa kale wa Palmyra

Mazungumzo hayo yaliahirishwa siku ya alhamisi huku mjumbe Staffan De Mistura akitangaza tarehe 9 mwezi Aprili kuwa siku ya kuanza tena mazungumzo hayo. Mjumbe wa upande wa serikali ya Syria katika mazungumzo hayo Bashar Ja'afari, alikutana na de Mistura hapo jana lakini hakuweka wazi kila walichokizungumzia.

Kwa upande wake George Sabra mwanachama mkuu katika akamati kuu ya upinzani amesema upande wake uko tayari kuendelea na mazungumzo. " Kupiga hatua katika mazungumzo haya ni ngumu lakini tutaendelea na juhudi za kutafuta muafaka," alisema George Sabra.

Syrien Kampf gegen IS
Mashambulio mjini PalmyraPicha: picture-alliance/dpa

Lakini wachambuizi wanasema iwapo rais Assad hataondoka madarakani kuna wasiwasi wa upinzani kujiondoa katika mazungumzo hayo mjini Geneva.

Huku hayo ya kiarifiwa ndani ya Syria kwenyewe vikosi vya serikali vimeingia katika mji wa kale wa Palmyra huku vikosi vya Iraq vikitekeleza mashambulizi mjini Mosul dhidi ya wanamgambo wa dola la kiislamu IS. Vikosi hivyo vcya Syria pia vinasaidiwa na vikosi vya kijeshi vya urusi kukabiliana na wanamgambo hao.

Kulingana na wizara ya Ulinzi ya Urusi, ndege zake za kivita zimefanya mashambulizi ya angani 146 katika maeneo ya wanamgambo hao kati ya jumapili na jumatano na kuwauwa magaidi 320.

Mwandishi: Amina Abubakar/AFP/AP

Mhariri: Yusuf Saumu