Haki ya kukusanyika majaribuni mkutano wa G20
5 Julai 2017Sheria hiyo itaingia majaribuni wakati viongozi wa nchi na serikali watakapokusanyika mjini Hamburg katika mkutano wa kundi la mataifa yaliyoendelea na yanayoinukia kiuchumi duniani G20.
"Kila Mjerumani ana haki , bila ya kujiandikisha ama ruhusa kutoka kokote kuweza kukusanyika kwa amani bila silaha." Hivyo ndivyo kinavyosema kifungu cha katiba ya Ujerumani aya ya 8. Hiki ni kifungu muhimu sana kukifahamu kabla ya kuanza kwa mkutano wa G20 mjini Hamburg siku ya Ijumaa . "Haki ya mkusanyiko wa aina hii inaweza kwa kupitia baadhi ya sheria ama kutokana na sababu za kisheria ikawekewa ukomo." Ni kutokana na kwamba hakuna sheria inayozuwia kutokuwa na ukomo katika sheria ya msingi.
Hii itatokana na maafisa wanapokaa vikao na kupata taarifa kutoka kwa polisi.
Vipi uhuru wa kukusanyika unaweza kutekelezwa , je sheria ya haki ya kukusanyika imepewa umuhimu na kudhibitiwa. Sheria hiyo imo katika vifungu 33. Mvutano kuhusiana na utekelezaji sahihi wa katiba iliyopitishwa na bunge la Ujerumani mwaka 1953 na kufanyiwa marekebisho mwaka 2008 ina husiana na utamaduni wa muda mrefu. Kwa kawaida machafuko ni kitu cha kawaida. Watayarishaji wanapinga sana kuwekewa masharti ama ukomo, katika wakati wa mkutano kama vile njia za kufanyia maandamano na kadhalika.
Maandamano yatafanyika lakini kwa masharti
Hali ya maandamano yenyewe pia ni suala ambalo limekuwa na mivutano mjini Hamburg kwa muda wa wiki kadhaa sasa. Kwasababu polisi wamezuwia wakati wa mkutano huo wa G20 kuanzia tarehe 7 hadi 8 Julai , eneo ambalo halitaweza kufikiwa katika siku zote hizo mbili ambalo linaukumbwa na kilometa za mraba 38 , na watu hawataruhusiwa kufika katika eneo hilo kwa ajili ya mkusanyiko wa aina yoyote.
Eneo hilo ni kutoka uwanja wa ndege kaskazini mwa mji huo hadi katika eneo la utawala katikati ya mji huo.
Eneo hilo litakuwa na ulinzi mkali , kutokana na uwezekano wa waandamanaji kujaribu kuzuwia barabara , ambayo inaelekea katika mkutano huo wa G20.
Kwa mtazamo wa polisi inaweza kuwa hatari kwa maisha ya viongozi wa mataifa , wanaoshiriki katika mkutano huo, polisi na watu wengine wanaohusika.
Pamoja na hayo mkutano huo wa G20 unaweza kuwa hatarini. Katika tathimini yao polisi wanasema hatari iliyopo , ilionekana pia katika mkutano wa kundi la mataifa yenye utajiri wa viwanda ya G8 mjini Heiligendam mwaka 2007 , katika mkutano wa NATO miaka miwili baadaye mjini Baden-Wuettemberg, maandamano ya kukalia mji mwaka 2014 ama kufunguliwa kwa benki kuu ya Ulaya EZB mwaka 2015 mjini Frankfurt am Main.
Mwanasheria wa serikali mjini Berlin Christian Pestalozza anasema inawezekana kubinya haki ya uhuru wa kukusanyika , kwasababu ya kuangalia usalama wa umma na utulivu. Suali lililopo ni kwamba ni hatua zinazochukuliwa katika kupunguza uhuru wa kujumuika au kukusanyika haliwezi kujibiwa kwa kusema ndio ama hapana alieleza mwanasheria huyo katika mazungumzo na DW.
Mwandishi: Marcel Fürstenau / ZR / Sekione Kitojo
Mhariri: Mohammed Khelef