1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroHaiti

Haiti yamteua Alix Didier Fils-Aimé kuwa Waziri Mkuu mpya

11 Novemba 2024

Baraza la mpito lililoundwa ili kurejesha utaratibu wa kidemokrasia nchini Haiti Jumapili lilisaini amri ya kumfukuza Waziri Mkuu wa muda nchini humo Garry Conille na nafasi yake kuchukuliwa na Alix Didier Fils-Aimé.

https://p.dw.com/p/4mr7s
Haiti | Waziri Mkuu Garry Conille
Waziri Mkuu wa Haiti Garry Conille aliyeondolewa na nafasi yake kupewa mtu mwingine, hatua inayoibua wasiwasi wa machafuko zaidi nchini humoPicha: Roberto Schmidt/AFP/Getty Images

Chanzo kimoja cha serikali kililiarifu Shirika la habari la Associated Press juu ya amri hiyo, inayotarajiwa kuchapishwa hii leo.

Hatua hiyo inatishia kuibuka mvutano zaidi katika mchakato huo wa kidemokrasia nchini humo.

Baraza hilo la mpito liliteuliwa mwezi Aprili na kupewa jukumu la kumchagua waziri mkuu na baraza la mawaziri litakalosaidia kutuliza mzozo nchini Haiti.

Hata hivyo baraza hilo limekuwa likikumbwa na mivutano ya kisiasa na baadhi ya wajumbe kukabiliwa na tuhuma za ufisadi.