1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Gwiji wa zamani wa Brazil Pele amtaka Putin kusitisha vita

2 Juni 2022

Gwiji wa zamani wa timu ya taifa ya Brazil ambaye anachukuliwa kuwa mmoja wa wachezaji bora duniani Pele amemtolea mwito rais wa Urusi Vladimir Putin kusitisha vita nchini Ukraine.

https://p.dw.com/p/4CBH0
Brasilien | Fußball-Legende Pele
Picha: Hans-Jürgen Schmidt/HJS-Sportfotos/picture alliance

"Komesha uvamizi,” Pele mwenye umri wa miaka 81 alisema katika barua ya wazi kwa Putin aliyoichapisha katika mtandao wa Instagram muda mfupi kabla ya mechi ya mchujo wa kombe la dunia kati ya Ukraine na Scotland Jumatano usiku. Scotland ilipata ushindi wa 3-1.

"Hakuna sababu yoyote ya msingi ya kuendelea na vita hivi,” aliongeza.

"Mgogoro huu ni mbaya, haukubaliki na hauna faida yoyote isipokuwa maumivu, hofu na uchungu. Hakuna sababu yoyote ya kurefusha vita hivi,” Pele ambaye ni mshindi mara tatu wa kombe la dunia katika miaka ya 1958, 1962 na 1970 alisema.

"Tulipokutana siku za nyuma na kutabasamu na kusalimiana kwa muda mrefu sikuwahi kufikiria kuwa tungegawanyika kama tulivyo sasa. Uwezo wa kukomesha mzozo huu upo mikononi mwenu. Mikono hiyo hiyo niliyoisalimia mjini Moscow katika mkutano wetu wa mwisho mwaka 2017.”

Ushindi wa timu ya taifa ya Ukraine uliisogeza timu hiyo katika fainali ya mechi ya mchujo dhidi ya Wales siku ya Jumapili huku mshindi akijikatia tiketi ya kushiriki michuano ya kombe la dunia litakaloandaliwa nchini Qatar.

Timu ya taifa ya Urusi ilipigwa marufuku kushiriki mechi za kufuzu michuano hiyo baada ya wanajeshi wake kuivamia Ukraine mnamo mwezi Februari.