Guterres ataka usitishaji mapigano Gaza, Sudan
11 Machi 2024Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa alitoa pia wito wa kuachiwa mateka wanaoshikiliwa na kundi la Hamas na kuondolewa kwa vizingiti vyote ili kuhakikisha upelekaji wa misaada ya dharura katika kasi na kiwango kikubwa kinachohitajika Gaza.
Soma zaidi: Umoja wa Mataifa wahofia mzozo wa Sudan kuongeza wakimbizi
Umoja wa Mataifa unaonya kuwa robo ya wakaazi wako ukingoni mwa kukabiliwa na njaa.
Wakati hayo yakijiri, Waziri wa Ulinzi wa Israel Yoav Gallan amesema mamlaka nchini humo zitaheshimu uhuru wa kuabudu wakati wa mfungo wa Ramadhani, lakini ziko "tayari" kwa mtu yeyote atakayevuruga amani.
Soma zaidi: Ramadhani yaanza bila usitishwaji vita Gaza
Kauli ya Yoav inatolewa wakati kukiwa na wasiwasi wa kutokea ghasia kipindi hiki cha Ramadhani katika Msikiti wa Al-Aqsa baina ya waumini wa Kiislamu na mamlaka za Israel.
Wapatanishi wa mzozo huo walitumai kupata muafaka wa kusitishwa mapigano kabla ya kuanza kwa kipindi hiki cha Ramadhani, lakini mpaka sasa hakuna mafanikio.