1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Guterres asema yuko tayari kufanya kazi na Donald Trump

7 Novemba 2024

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema yuko tayari kufanya kazi na rais mteule wa Marekani Donald Trump licha ya wasiwasi kwamba muhula mpya wa Trump utarejesha mbinyo kwenye chombo hicho cha ulimwengu.

https://p.dw.com/p/4mj2E
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres.Picha: REUTERS

Kwenye taarifa iliyotolewa na ofisi yake, Guterres amejiunga na viongozi wengine duniani kumpongeza Trump kwa ushindi aloupata na kusisitiza kwamba ushirikiano kati ya Marekani na Umoja wa Mataifa ni nguzo muhimu kwenye mahusiano ya kimataifa.

Muhula wa kwanza wa Trump madarakani ulishuhudia mashambulizi ya kila wakati dhidi ya Umoja wa Mataifa na hata kupunguzwa kwa ufadhili wa kibajeti unaotolewa na Washington kwenye chombo hicho.

Vilevile msimamo wa Trump wa kutanguliza maslahi ya Marekani kwanza uliteteresha uthabiti wa mahusiano ya kimataifa hasa katika kuzishughulikia changamoto za kilimwengu.