1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaKorea Kusini

Guterres aonya kutumika kwa wanajeshi wa Pyongyang, Ukraine

4 Novemba 2024

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameelezea wasiwasi kuhusu uwezekano wa kupelekwa kwa wanajeshi wa Korea Kaskazini katika uwanja wa vita nchini Ukrane.

https://p.dw.com/p/4mYNo
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akihutubia mkutano wa 79 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York mnamo Septemba 24,2024
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio GuterresPicha: REUTERS

Taarifa ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa Jumapili mjini New York nchini Marekani, imesema uwezekano wa kutumika kwa wanajeshi hao wa Korea Kaskazini utasababisha ongezeko la hatari la vita hivyo nchini Ukraine na kuongeza kuwa hatua zote zinapaswa kuchukuliwa kuepusha kutanuka kwa mzozo huo kimataifa.

Korea Kaskazini yasema inaiunga mkono Urusi hadi mwisho

Katibu huyo mkuu alisisitiza kuhusu uungaji wake mkono kwa juhudi zozote muhimu kuelekea amani ya haki na ya kudumu nchini Ukraine, kwa mujibu wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa, sheria za kimataifa na maazimio ya Baraza Kuu la Umoja huo.

Takriban wanajeshi 8,000 wa Pyongyang wadaiwa kuwa Urusi

Kulingana na Marekani, takriban  wanajeshi 8,000 wa Korea Kaskazini wamepelekwa katika eneo la karibu na mpaka wa Ukraine na huenda wakaanza kutumiwa na Urusi kwenye vita nchini humo katika siku zijazo.