Guinea ya Ikweta yaiomba ICJ kuyakataa madai ya Gabon
30 Septemba 2024Matangazo
Nchi hizo jirani na wazalishaji wa mafuta barani Afrika zimeiomba mahakama ya ICJ kuusuluhisha mzozo wa muda mrefu kuhusu kisiwa kidogo cha Mbanié kilicho kwenye pwani ya Gabon na chenye ukubwa wa chini ya kilomita moja.
Mzozo huo umekuwa ukiendelea tangu mwaka 1972, wakati jeshi la Gabon lilipowafukuza wanajeshi wa Guinea ya Ikweta kutoka Mbanié.
Soma zaidi: Kiongozi wa kijeshi wa Gabon ziarani Burundi
Kwa upande wake, tangu wakati huo Gabon imewaweka wanajeshi wake kwenye eneo hilo lisilo na watu kwenye kisiwa hicho chenye ukubwa wa ekari 74 tu.
Mahakama ya mjini The Hague inatarajiwa kutoa uamuzi wake mwaka ujao.