1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Guinea kuanza kuwachanja watoto dhidi ya COVID-19

10 Novemba 2021

Guinea itaanza kuwachanja leo watoto wa chini ya umri wa kati ya miaka 12 na 17 dhidi ya ugonjwa wa UVIKO-19 kwa kutumia shehena za chanjo za Pfizer na Moderna.

https://p.dw.com/p/42oR4
Corona Impfstoff Moderna Biontech Pfizer
Picha: CHRISTOF STACHE AFP via Getty Images

Nchi nyingi za Kiafrika zimekuwa zikitegemea mpango wa kugawana chanjo wa COVAX, na zimetoa chanjo kwa sehemu ndogo tu ya raia wao.

Guinea ilipokea chanjo za Pfizer/BioNTech na Moderna mwishoni mwa Oktoba na mapema Novemba.

Taarifa ya Shirika la Kitaifa la Usalama wa Kiafya halijasema ni kiasi gani cha dozi zilitolewa na kutoka wapi.

Guinea imetoa karibu dozi 2,276,474 za chanjo ya UVIKO-19 mpaka sasa, ambazo zinatosha kuwachanja kikamilifu karibu asilimia 9 ya raia wake, kwa mujibu wa data za serikali.