Gianni Infantino achaguliwa tena rais wa FIFA
16 Machi 2023Infantino, raia wa Uswisi, mwenye umri wa miaka 52, alithibitishwa kuendelea na wadhfa wake huo kwa shangwe katika kongamano la FIFA linalofanyika mjini Kigali, Rwanda.
Infantino, amechaguliwa tena kwa mara ya kwanza tangu achukue wadhifa huo kwenye muhula uliosalia wa mtangulizi wake Joseph Blatter aliyesimamishwa mwaka 2016.
Infantino: Mizozo ikome wakati wa kombe la dunia
Kulingana na sheria za FIFA, hii ina maana kwamba anaweza kugombea muhula mwingine kuanzia mwaka 2027 hadi 2031.
Infantino anaungwa mkono kwa wingi na wanachama wa FIFA lakini pia nchi kadhaa za Ulaya zikiwemo Ujerumani, Norway na Uswisi hazifurahishwi na yeye kuwa rais wa FIFA na zimesema hazitamuunga mkono kikamilifu.
Infantino amesema baada ya kuthibitishwa kwamba anawapenda wote wanaompenda, ambao ni wengi la pia wachache wanaomchukia. Amesema kuwa rais wa FIFA ni heshima na fursa kubwa, lakini pia ni wajibu mkubwa na kwamba watu waendelee kuamini ahadi yake.