GENEVA: Vikosi vya dharura kusaidia wakimbizi
20 Machi 2005Matangazo
Umoja wa Mataifa uliolaumiwa kuwa unachelewa kuchukua hatua inapozuka mizozo,sasa unataka kuwa na kikundi cha wasaidizi kitakachoweza kupelekwa kwa haraka kushughulikia mahitajio ya dharura ya wakimbizi kama vile huko Darfur nchini Sudan.Mratibu wa misaada ya dharura ya Umoja wa Mataifa Jan Egeland amesema,pendekezo hilo linaungwa mkono na wafadhili wengi kama vile Uingereza,Marekani na nchi za Skandinavia.Egeland amesema vikosi vya aina hiyo vingeweza kuzuia mauaji na ubakaji ulioongezeka mwaka jana katika jimbo la magharibi la Darfur nchini Sudan.Huko takriban wakimbizi milioni mbili wanakabiliana na hatari ya kushambuliwa na wanamgambo wa Janjaweed,waasi na vikosi vya serikali alieleza Egeland.