GENEVA: Usalama wa ndege za Flash mashakani
5 Januari 2004Matangazo
Kufuatia ajali ya kuangukwa kwa ndege kwenye Bahari Nyekundu ambayo imeuwa watu 148 rekodi ya usalama ya shirika la ndege la kukodiwa la Misri imeanza kutiliwa mashaka. Wafanyakazi wa uwanja wa ndege mjini Geneva na Athens wamesema ndege mbili za Shirika hilo la Flash zilituwa kwa dharura kutokana na sababu za kiufundi katika kipindi cha miaka miwili iliopita.Swirtzerland imethibitisha kwamba imezipiga marufuku ndege za Shirika la Ndege la Flash kutuwa au kuruka juu ya anga yake kutokana na mashaka ya usalama.Ndege hiyo ya Shirika la Ndege la Flash Boeing 737 ilikuwa njiani ikitokea mji wa kitalii wa Bahari Nyekundu wa Sharm el Sheikh nchini Misri wakati ilipoanguka na kutumbukia baharini. Juhudi za kutafuta visanduku viwili vya kurekodia nyendo za safari za ndege hiyo bado zinaendelea.