GENEVA: Umoja wa mataifa waagiza uchunguzi tena wa kifo cha Hariri.
25 Machi 2005Umoja wa Mataifa umeagiza uchunguzi mpya wa kimataifa ufanyike kutafuta chanzo cha mauaji ya aliyekuwa waziri mkuu wa Lebanon Rafik Hariri.
Agizo hilo limefuatia ripoti ya wachunguzi wa umoja wa mataifa kuhusu kifo cha Hariri ya kwamba uchunguzi wa hapo awali ulijawa na ushawishi na visa udanganyifu.
Katika mkasa huo majeshi ya Syria yaliyohudumu nchini Syria yamelaumiwa kwa kutowajibika vilivyo kutoa ulinzi wa kutosha na kufuata sheria za serikali ya Lebanon.
Walebanon wengi wanailimbikizia Syria lawama za kifo cha Rafik Hariri aliyeuwawa katika mlipuko wa bomu ndani ya gari katika mji wa Beirut.
Rais Emile Lahud wa Syria amelikubali pendekezo la tume ya kimataifa ya kuchunguza kifo cha Hariri.
Na wakati huo huo Balozi wa Syria katika Umoja wa Mataifa Faysal Mekdad amekataa katakata kuwa Syria inahusika na mauaji ya Rafik Hariri.