1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GENEVA: Shirika la WHO lasema sampuli za virusi zinakosekana

16 Aprili 2005
https://p.dw.com/p/CFMe

Kwa mujibu wa WHO-Shirika la Afya Duniani la Umoja wa Mataifa,takriban maabara zote kutoka 3,700 zilizopokea sampuli za virusi hatari kabisa vya flu,zimeshateketezwa.Lakini mwanasayansi mkuu wa WHO,bwana Klaus Stohr amewaambia maripota mjini Geneva kuwa maabara nchini Mexico na Lebanon zilizokuwemo kwenye orodha,hazikupokea sampuli hizo.Virusi hivyo ni sawa ni vile virusi vya flu vya mwaka 1957,vilivyouwa hadi watu milioni 4 kote duniani.Sampuli hizo zilitumwa na Chuo cha Kimarekani cha wataalamu wanaochunguza asili na matokeo ya magonjwa.