1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GENEVA: Shirika la afya duniani laidhinisha mpango wa kupambana na homa ya ndege

10 Novemba 2005
https://p.dw.com/p/CEJv

Shirika la afya duniani, WHO, limeidhinisha mpango wa kupambana na kuenea kwa homa ya ndege utakaogharimu kiasi cha dola bilioni moja. Wataalamu wa afya kutoka mataifa zaidi ya 100 waliutayarisha mpango huo katika kikAo chao cha siku tatu mjini Geneva. Mkutano wa kuchagisha fedha kwa ajili ya mpango huo umepangwa kufanyika mjini Beijing mwezi Januari mwakani.

Mpango huo unalenga kuboresha mbinu za kuonya dhidi ya homa ya ndege, kuhakikisha dawa za kupambana na virus wanaosababisha homa hiyo zinapatikana bila vikwazo, na kuongeza utafiti wa kutafuta chanjo dhidi ya homa hiyo.

Virusi aina ya H5N1 wamesababisha vifo vya watu 60 barani Asia. Wataalamu wanahofu virusi hao wanaweza kubadili umbo lao na kuingia katika mwili wa binadamu, hivyo kuzusha janga kubwa.