1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GENEVA: Rwanda yapiga marufuku adhabu ya kifo

28 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBeW

Uamuzi wa Rwanda kuondosha adhabu ya kifo umekaribishwa na Umoja wa Mataifa na Amnesty International,shirika linalogombea haki za binadamu duniani.Kamishna wa Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa,Bibi Louise Arbour amesema,hatua hiyo inafungua njia ya kuwafikisha mahakamani washukiwa mauaji ya halaiki nchini humo,ambako kiasi ya watu 800,000 waliuawa katika mwaka 1994.Shirika la Amnesty International limesema,Rwanda imekuwa nchi ya kwanza katika kanda ya Maziwa Makuu,kupiga marufuku adhabu ya kifo na kuthibitisha mwenendo wa dunia nzima,kukomesha adhabu ya kifo.