GENEVA: Rais wa uswisi afungua mkutano wa mawasiliano yanayotumia mitambo ya kisasa
10 Desemba 2003Matangazo
Mda mfupi uliopita, Rais wa Uswisi Pascal Couchepin, amefungua mkutano wa kimataifa wa mawasiliano ya kisasa, ya kutumia Internet na computer.
Mkutano huo unalenga kupunguza pengo lililoko wakati huu, kuhusu idadi ya watu wenye uwezo wa kutumia na kufaidika kwa mawasiliano ya aina hiyo, katika nchi zilizoendelea, na nchi masikini.
Wanahudhuria mkutano huo, wajumbe kutoka nchi miamoja sabini na tano, wakiwemo wakuu wa nchi na serikali, zaidi ya arbaine.
Katika mijadala iliyokuwepo leo asubuhi kabla ya kuanzishwa rasmi mkutano huo, baadhi ya wajumbe wamelalamika dhidi ya uamuzi kwamba mkutano ujao wa aina hiyo kufanyika nchini Tunisia mwaka wa 2005, wakati ambako nchi hiyo ni miongoni mwa nchi zisizoheshimu uhuru wa msemo na wa vyombo vya habari.
Katibu mkuu wa shirika la kimataifa la kutetea haki ya uhuru wa vyombo vya habari, Bwana Robert Ménard, amesema ni jambo la aibu, kwamba nchi ambayo ni miongoni mwa nchi ishirini zenye umaarufu wa kukandamiza vyombo vya habari, inachaguliwa kuwa mwenyeji wa mkutano ujao wa mawasiliano ya kutumia Internet.