GENEVA: Nzige na ukame kitisho kwa mavuno nchini Niger
29 Mei 2005Matangazo
Taifa la Niger lililokumbwa na ukame,limetoa wito wa kupewa msaada wa dharura wa chakula kwa ajili ya mamilioni ya watu wanaokabiliwa na upungufu mkubwa wa chakula.Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, kiasi ya watu milioni 3.6 wanahitaji msaada wa dharura.Umoja huo umeitaka jumuiya ya kimataifa itoe msaada wa Euro milioni 13 kugharimia kile kilichoitwa „msiba usiotajwa“.Nzige waliotapakaa nchini Niger vile vile wanahatarisha zaidi uwezekano wa kupata mavuno mazuri.Familia nyingi katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi,ambayo ni miongoni mwa nchi zilizo masikini kabisa, hutegemea mashamba yao kwa chakula.