1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GENEVA : Nchi tajiri zijitahidi zaidi kupiga vita umasikini

11 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCkR

Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa linalotetea haki za binadamu,Louise Arbour ameyatuhumu mataifa tajiri kuwa hayajitahidi vya kutosha kupiga vita umasikini.Jumapili,alipozungumza mjini Geneva,kuadhimisha siku ya haki za binadamu duniani,Bibi Arbour alisema,matumizi ya serikali kwa ajili ya silaha na ruzuku za kilimo,yapangwe upya kwa manufaa ya misaada ya maendeleo na vita dhidi ya umasikini.Amesema,matumizi ya kijeshi ni mara kumi zaidi ya zile pesa zinazotumiwa kupiga vita umasikini.