Geneva: Mkataba wa amani wa ishara umetiwa saini:
2 Desemba 2003Wanasiasa wa Kipalestina na Kiisraeli wametia saini mkataba wa amani wa ishara usiotambuliwa rasmi na serikali za Israeli na Palestina. Pande zote mbili zina hiari ya kuchunguza mkataba huo wa kibinafsi ambao ni mfano wa mkataba rasmi unaoweza kufikiwa kati yao. Dhana muhimu ni kuanzishwa kwa nchi ya Wapalestina na mji wa Jerusalem kugawika katika sehemu mbili. Israeli italazimika kurudi nyuma katika ile mipaka iliyokuwapo kabla ya vita vya siku sita vya mwaka 1967. Wapalestina kwa upande wao wanapaswa kuitambua rasmi Israeli na wale waliopoteza ardhi zao ambazo sasa ziko mikononi mwa Waisraeli wasizidai tena baada ya kurudi kwao. Mkataba ishara wa Geneva unaungwa mkono na Watunukiwa kadhaa wa tunzo la amani la Nobel. Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Ujerumani, Joschka Fischer, amezungumzia kuhusu mchango wa kishujaa wa kumaliza mgogoro wa Mashariki ya Kati.