1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GENEVA: Misaada yatiririka Lebanon

14 Agosti 2006
https://p.dw.com/p/CDLb

Mashirka ya kutoa misaada ya kiutu yameongeza juhudi zao za kuwapelekea misaada wahanga wa vita kusini mwa Lebanon, baada ya mapigano kati ya wanajeshi wa Israel na wanamgambo wa kundi la Hezbollah kusitishwa.

Msemaji wa ofisi ya uratibu wa misaada ya Umoja wa Mataifa mjini Geneva, Uswisi, Elisabeth Byrs, amesema misafara ya magari ya maashirika kadhaa ya misaada yaliyosheheni vyakula na tani takriban 100 za mafuta, imo njiani kuelekea kusini mwa Lebanon.

Misafara mingine mitatu ya malori 24 yaliyobeba maji ya kunywa, vyakula, dawa na mahitaji mengine yanaelekea mjini Sidon, huku mengine yakielekea mji wa Jezzine, katikati mwa Lebanon.

Wakati huo huo, kundi la Hezbollah linashangalia ushindi mubwa mtakatifu dhidi ya Israel. Mbunge wa Hezbollah, Hassan Fadlallah amesema wanamgambo wa kundi lake watarejea nyumbani wakiwa mashujaa kwa kufaulu kuizuia Israel.

Israel kwa upande wake inasema imeshinda kwa kuwa kundi la Hezbollah haliwezi tena kufanya ilitakalo nchini Lebanon.