1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GENEVA : Milioni 89 zaidi kuwa wahanga wa UKIMWI Afrika

4 Machi 2005
https://p.dw.com/p/CFZf

Watu wengine milioni 89 zaidi barani Afrika wanaweza kuabukizwa na virusi vya HIV ifikapo mwaka 2025 venginevyo dunia inachukuwa hatu kali kuudhibiti ugonjwa huo wa UKIMWI katika bara lilioathirika vibaya na maambukizi yake.

Hiyo ni mojawapo ya hali mbaya kabisa zilizotabiriwa kwenye repoti ya shirika la Umoja wa Mataifa la kushughulikia UKIMWI UNAIDS ambalo linatabiri kuongezeka vifo mara nne zaidi kutokana na gonjwa hilo thakili katika kipindi cha miaka 20.

Kwa mujibu wa repoti hiyo hata kama kutakuwepo na mipango mizuri ya kudhibiti UKIMWI kwa gharama za dola bilioni 200 maambukizi mapya ya watu milioni 46 yanatabiriwa kutokea Afrika katika kipindi hicho.

Takriban watu milioni 25 kusini mwa Jangwa la Sahara tayari wanaishi na virusi vya HIV na UKIMWI ikiwa ni sawa na asilimia 70 ya jumla ya watu walioambukizwa ugonjwa huo duniani.