1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GENEVA: Migogoro imeongeza wakimbizi duniani

19 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBqJ

Idadi ya wakimbizi duniani imeongezeka kwa mara ya kwanza,baada ya miaka mitano.Kwa mujibu wa ripoti ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa leo hii, watu wanaoikimbia Iraq iliyoteketezwa kwa vita, imechangia kuongezeka kwa idadi ya wakimbizi duniani.Mkuu wa Shirika linaloshughulikia wakimbizi-UNHCR amesema,kote duniani sasa kuna wakimbizi milioni 9.9.Hadi mwisho wa mwaka 2006, Wairaqi milioni 1.5 walikimbilia nchi za ngámbo. Vile vile,idadi ya watu waliopoteza makazi yao katika nchi zao imeongezeka hadi 20.5.Mbali na Iraq,migogoro ya nchini Lebanon, Timor ya Mashariki,Sudan na Sri Lanka imelaumiwa kusababisha kuongezeka kwa idadi ya wakimbizi duniani.