1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GENEVA : Mazungumzo ya amani ya Sri Lanka yavunjika

30 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CCxs

Mazungumzo ya siku mbili ya amani ya Sri Lanka yamesambaratika mjini Geneva baada ya pande mbili zinazohasimiana kushindwa kukubaliana juu ya tarehe ya kuanza upya kwa mchakato huo.

Msuluhishi mkuu wa Norway Erik Solheim amewaambia waandishi wa habari kwamba wawakilishi wa serikali ya Sri Lanka na waasi wa kundi la Tamil Tiger wameshindwa kukubaliana juu ya jinsi ya kushughulikia masuala muhimu ya kibinaadamu.Pande zote mbili hazikuahidi kudumisha makubaliano ya amani yanayodhoofika waliyofikia mwaka 2002 juu ya kwamba yamekuwa yakikiukwa sana katika miezi ya hivi karibuni.

Suala kuu kwaTamil Tiger lilikuwa ni kushughulikia mahitaji ya kibinaadamu ya Watamil walioathirika kutokana na mapigano ya hivi karibuni na kufunguliwa tena kwa barabara kuu pekee yenye kuingia kwenye rasi ya kaskazini ya Jaffna.