GENEVA: Marekani na Korea Kaskazini zakaribia kuafikiana
1 Septemba 2007Matangazo
Wajumbe wa Marekani na Korea Kaskazini wameanza majadiliano ya siku mbili katika mji wa Geneva nchini Uswissi.Azma ya mazungumzo hayo ni kufungua njia ya kupata makubaliano kuhusu mradi wa silaha za nyuklia wa Pyongyang na kusawazisha uhusiano kati ya nchi hizo mbili.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani,Christopher Hill ambae pia ni mpatanishi mkuu wa Marekani amesema,ni matumaini yake kuwa makubaliano yatapatikana wakati wa mazungumzo ya pande hizo mbili. Marekani inatumaini kuwa Korea Kaskazini itasitisha mradi wake wa silaha za nyuklia ifikapo mwisho wa mwaka huu.