GENEVA: Marekani lazima ifunge jela za siri
29 Julai 2006Halmashauri ya Umoja wa Mataifa inayotetea haki za binadamu duniani,imetoa mwito kwa Marekani ifunge jela zake zote zinazoendeshwa kwa siri.Mwito huo umetolewa katika ripoti iliyozusha wasi wasi kuhusu njia zinazotumiwa kupiga vita ugaidi.Halmashauri hiyo imeitaka Marekani pia ikiruhusu chama cha kimataifa cha Msalaba Mwekundu kuonana na wale wanaozuiliwa katika jela za aina hiyo.Ripoti ya Umoja wa Mataifa vile vile imeshughulikia hali ya haki za binadamu nchini Marekani.Serikali ya Marekani,imehimizwa kuhakikisha kuwa haki za masikini na Wamarekani weusi zinaheshimiwa katika juhudi za kutoa misaada.Wakati huo huo,ripoti imeamua kuwa adhabu ya kifo yapaswa kuahirishwa-ikidhihirika kwamba adhabu hiyo hutolewa bila ya uwiano kwa makundi ya walio wachache na watu masikini.