GENEVA: Marekani itawachukua wakimbizi 10,000 wa Burundi kutoka Tanzania
18 Oktoba 2006Matangazo
Marekani imepanga kuwachukua wakimbizi takriban 10,000 wa Burundi kutoka Tanzania.
Umoja wa mataifa uliomba wapelekwe nchini Marekani mnamo miaka michache ijao. Marekani itawapatia hati ya kudumu kukaa nchini humo, ikiwa ni hatua ambayo huenda ikawafikisha kupata uraia.
Wakimbizi hao wa Burundi watakaopelekwa nchini Marekani, ni miongoni mwa maelfu ya wakimbizi wa kihutu walioyatoroka mauaji ya mwaka wa 1972.
Maelfu ya ma mia wengine waliyakimbia machafuko katika kipindi cha miaka 12 ya vita vya wenyewe kwa wenyewe ambapo kiasi ya watu laki tatu waliuawa kabla ya mzozo huo kumalizika mwaka uliopita kwa mkataba wa amani unaosimamiwa na kikosi cha kijeshi cha kulinda amani cha Umoja wa mataifa.