GENEVA : Makubaliano ya bishara duniani yako njiani
15 Novemba 2007Nchi zinazoendelea zimesema leo hii kwamba makubaliano yaliofanikiwa ya biashara duniani yako njiani kufikiwa licha tafauti kubwa zilioko na nchi zenye maendeleo makubwa ya viwanda juu ya kilimo na kuhitilafiana juu ya bidhaa za viwandani.
Mawaziri wanane kutoka nchi za kundi la mataifa manane yenye maendeleo makubwa ya viwanda wakiwemo pia wa nchi za India,Afrika Kusini,Argentina na Tanzania wanakutana makao makuu ya Shirika la Biashara Duniani chini ya ombi la waziri wa mambo ya nje wa Brazil Celso Amorim ambaye ni mjumbe mkuu wa biashara wa nchi hiyo.
Kundi la mataifa 20 yanayoinukia kiuchumi duniani limesema kwenye taarifa kwamba kundi lao liko tayari kuendeleza mazungumzo ya tija na katika kutatuwa matatizo na nchi nyengine wanachama wa WTO ili kuingia kwenye mazungumzo ya mwisho.
Mazungumzo ya duru ya Doha ya miaka sita juu ya kupunguza vikwazo vya biashara kwa bidhaa za kilimo, viwanda na kutowa huduma bado ingali yamekwama licha ya kufanyika kwa mazungumzo hayo mara kadhaa katika makao makuu ya Shirika la Biashara Duniani WTO mjini Geneva.