GENEVA. El Baradei achaguliwa tena
14 Juni 2005Matangazo
Nchi 35 wanachama wa shirika la kimataifa la nguvu za atomiki zimepitisha kwa kauli moja kura ya kumchagua bwana Mohamed el Baradei kuliongoza kwa kipindi kingine shirika linalofuatilia maswala ya kinuklia la umoja wa mataifa.
Utawala wa rais Bush wa Marekani ulibadili nia yake ya kumpinga bwana El Baradei wiki iliyopita licha ya tofauti zilizokuwepo katika tathmini juu ya Iraq na Iran.